Kwa unyenyekevu twende sote, yeye (Bwana
Yesu) ametualika (sote) tule mwili wake tunywe damu yake tupate uzima (huo wa) milele
1.Ni karamu ya upatanisho,
  atualika twende sote –
twende ndugu twende
  Karamuye yaleta amani,
  tuishi kwa upendo wake –
twende ndugu twende
2.Ndugu ujitayarishe kweli,
  kumpokea Yesu Mwokozi –Â
  Tule mwili tunywe damu pia,
  kwa ukumbusho wake Kristu –
3.Bwana kwa upendo wake mkuu,
  mema ya mbingu ametupa –
  Tumejazwa na neema zake,
  baraka za mbingu twapata –
4.Heri wale waulao mwili,
  na kuinywa damu ya Yesu –
  Chakula hiki ni cha uzima,
  tukila twaishi milele –