1.Twawashangilia hawa wenzetu,
  kwa uamuzi wao kuifunga ndoa – Hoye hoye, hoye hoye
  Tunawapongeza, tunawatakia heri njema
  Ni dhihirisho tosha kweli mwapendana -  tunawatakia heri njema
  Huu ni mfano bora wa penzi la dhati - tunawatakia heri njema
2.Hii ni siku yenu mliyotengewa,
  bwana na bibi harusi mfurahie – Hoye hoye, hoye hoye
  Tunawapongeza, tunawatakia heri njema
  Mungu awajalie muwe na watoto - tunawatakia heri njema
  Na pia muwafunze kumwogopa Mungu - tunawatakia heri njema
3.Bwana harusi umpende mkeo,
  nawe bibi harusi umheshimu mumeo – Hoye hoye, hoye hoye
  Tunawapongeza, tunawatakia heri njema
  Na msameheane panapo makosa - tunawatakia heri njema
  Panapo tofauti mtatue kwa amani - tunawatakia heri njema
  Uamuzi wenu kweli wapendeza, machoni pa Mungu na viumbe vyake
  Mlilolitenda kweli linafaa, dhihirisho tosha kweli mwapendana
  Hoye hoye, hoye hoye, hoye hoye, hoye hoye
  Tunawatakia heri njema x3