[Bwana ndiye mchungaji (Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu) x2] x2
 1.Kwenye malisho ya majani, kwenye malisho ya majani mabichi hunilaza,
  kando ya maji matulivu - kando ya maji matulivu huniongoza
2.Hunihuisha nafsi yangu, hunihuisha nafsi yangu na kuniongoza,
  katika njia za haki - katika njia za haki kwa’jili ya jina lake
3.Naam nijapopita kati, ya bonde la uvuli wa mauti sitaogopa,
  mabaya Wewe u pamoja nami - gongo lako na fimbo yako vyanifariji
4.Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu wanipaka mafuta,
  umenipaka mafuta – kichwani pangu na kikombe changu kinafurika
 5.Hakika wema na fadhili, zitanifuata siku zote za maisha yangu,
  nami nitakaa nyumbani - nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele