UTUKUFU - FR. P. ASSENGA, A.J
(Utukufu kwa Mungu juu, utukufu kwa Mungu juu mbinguni, (na amani) na amani na amani duniani kwa watu, kwao watu aliowaridhia.)*2
Tunakusifu (Ee Bwana) Tunakusifu
Tunakuheshimu
Tunakuabudu (Bwana)
Tunakutukuza.
(Bwana) Tunakushukuru (Bwana) kwa ajili ya utukufu wako mkuu, ee Bwana Mungu Mfalme: Mfalme wa mbinguni, Mungu Baba Mwenyezi (Ee Bwana).
Ee Bwana Yesu Kristo Mwana wa pekee, ee Bwana Mungu,
Mwanakondoo wa Mungu, Mwana wa Baba,
Mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu, (Bwana) utuhurumie.
Mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu (Bwana) pokea ombi letu.
Mwenye kuketi kuume kwa Baba, utuhurumie. Kwa kuwa ndiwe, uliye peke yako, Mtakatifu (Bwana) peke yako Bwana, peke yako uliye juu kabisa, Yesu Kristo.
Pamoja naye Roho, Roho Mtakatifu, Katika utukufu wa Mungu Baba, Amina.
(Amina, Amina, Amina, Amina, Amina.)*2