1.Salamu ee Mama Maria wanao twakusalimu –
Salamu Maria
  Bikira Mama wake Mungu Mama wa Mwokozi wetu –
Salamu Maria
Heshima tunazitoa kwako (mstaajabivu) Mama (mpendelevu) sisi tunakusalimu
Kizazi hadi kizazi 'Wewe (mbarikiwa)' kweli (vitataja) sisi tunakusalimu
2.Umebarikiwa Maria Mama umejaa neema –
 Tunakupongeza Mama kutuzalia Mkombozi –
3.Kutaja sifa za Maria mimi kamwe sitaacha –
  Mama usiye na doa Mama usiye nazo dhambi -
4.Kioo cha haki kikao cha hekima mlango wa mbingu -
  Chombo cha neema na heshima chombo bora cha ibada –
5.Malkia uliyezaliwa pasipo dhambi ya asili –
  Afya ya wagonjwa hizo baadhi za sifa zako Mama -