NI NENO JEMA KUMSHUKURU BWANA (Zab 92)
[
Nd. Stanslaus L. Mkombo, OFMCap
]
//
Ni neno je---ma kumshukuru Bwana, (Mungu wetu) na kuliimbia Jina lako ee Uliye Juu, kuzitangaza rehema zako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku
.//x2
1.   Â
I: Kwa chombo chenye nyuzi kumi, kwa kinanda na kwa mlio wa sauti tamu ya kinu-bi;
(I-IV) Umenifurahisha Bwana, kwa kazi ya mikono yako; na kwa matendo yako nitashangilia.
2.    II: Wasio haki wataangamizwa milele, maana hao adui zako Bwana watapotea;
(I-IV) Watendao maovu watatawanyika wote pia.
3.   Â
III: Lakini mwenye haki atasitawi kama mtende, atakuwa kama mwerezi wa Lebanoni;
(I-IV) Waliopandwa nyumbani mwa Bwana watasitawi katika nyua zake.
4.   Â
IV: Watazaa matunda hata wakati wa uzee, watajaa utomvu watakuwa nao ubichi; watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili,
(I-IV) Ndani yake Mwamba wangu hamna udhalimu.