KIITIKIO
Ndipo ghafla, ndipo ghafla, ndipo ghafla x2
Ndipo ghafla ikaja sauti ya ngurumo;
Ngurumo,ngurumo,ngurumo, mithili ya upepo wenye nguvu x2
Ukaijaza nyumba yote, ukaijaza nyumba yote walipokuwa wamekaa, walipokuwa wamekaa x2
Wote wakajazwa na Roho,wote wakajazwa na Roho,(hao) wote wakajazwa na Roho,(hao) wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wakisema matendo makuu ya Mungu Aleluya.
Atukuzwe Baba na Mwana, atukuzwe Baba na Mwana, atukuzwe Baba na Mwana naye Roho Mtakatifu x2
MASHAIRI
Inakuwaje tunasikia maneno yanayosemwa,kwa lugha yetu wenyewe kwa lugha yetu wenyewe.
Mungu Baba Mwana naye Roho atukuzwe siku zote kwa shangwe aabudiwe siku zote atukuzwe.
Twendeni sote leo njoni twendeni tutangaze neno la Mungu kwa mataifa yote.tulipeleke  kwa watu wote watamaduni na lugha zote kadiri ya Roho Mtakatifu atakavyotuezesha kutangaza neno lake,neno lienee pote.