Leo amezaliwa kwa ajili yetu Mwokozi, Ndiye Kristo Bwana ndiye Kristo Bwana, ndiye Kristo Bwana ndiye Kristo Bwana x2.
1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya.
Mwimbieni Bwana nchi yote.
Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake.
2. Tangazeni wokovu wake siku kwa siku
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake
Na watu wote habari za maajabu yake.Â
3. Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,
bahari na ivume na vyote viijazavyo,
Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,
ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha.Â
4. Mbele za Bwana, kwa maana anakuja,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki,
na mataifa kwa uaminifu wake.