Leo hii wakristu leo hii twendeni tumwabudu Bwana hekaluni
Ni siku ya Bwana na imetakaswa twendeni (na) twendeni – tumfanyie shangwe Mfalme wa dunia na pia mbinguni
Hekaluni mwake – tupate baraka zake Bwana Mungu njoni leo njoni na tumwabudu
1.Twende kwake Bwana ni Mungu wetu –
Twende kwa heshima na tumwabudu
  Twende kwake Bwana Mfalme wetu –
  Twende kwake Bwana Mlinzi wetu –
2.Nyumbani mwa Bwana nyumba ya sala –Â
Nafsi ifurahi katika Bwana
  Kwa heshima twende tukamwabudu –
  Tupate neema na msamaha –
3.Sisi ni kondoo wa malishoye –
Anatujalia ni Baba yetu
  Katufanya sisi tupate shibe –
  Ndiye atupaye na afya njema –
4.Sifa na heshima ni vyake Mungu –
Yeye Mungu wetu anastahili
  Mbingu na dunia ni Mtawala –
  Utukufu wote wake na enzi –