ENYI TAIFA LA MUNGU NJOONI
Mtunzi:
Dr. Basil Tumaini
Kiitikio
: Enyi Taifa la Mungu njooni, njoni tumwimbie Mungu, njoni tumshukuru.
       Bwana ninakushukuru kwa neema zako nyingi unazonijalia Bwana asante.
Viimbizi
(
chagua mashairi unayotaka kuimba
):
1. Na kwa
uhai
nilionao (Mungu wangu) kwa
afya njema
nakushukuru Ee Bwana Mungu asante.
2. Kwenye
familia
tulizonazo (Mungu wetu)
Upendo
wako ukatawale Ee Bwana Mungu asante.
3. Katika raha katika shida (Mungu wangu)
Uko daima, u kimbilio
Ee Bwana Mungu asante.
4.
Kanisa lako
waliongoza (Mungu wetu) Liwe imara lisimamie Ee Bwana Mungu asante.
5. Kwa
Mwili wako
, kwa
Damu yako
(Mungu wetu) Umejitoa kutushibisha Ee Bwana Mungu asante.
6. Yanatimia malengo yangu (Mungu wangu)
mafanikio
ninayapata Ee Bwana Mungu asante.
7. Nayo
amani
nchini mwetu (Mungu wetu) Tunakuomba uidumishe Ee Bwana Mungu asante.
8. Na siku hii ni
kumbukumbu
(Mungu wangu) Ya wema wako wewe Mwenyezi Ee Bwana Mungu asante.
9. Na kwa kinanda na matoazi (na kayamba) sauti tamu nitapaaza
kukushukuru Ee Mungu
.