Ee Bwana Fadhili zako ni za milele ((K): Zab. 137:8) Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini (0767 847 258)
Kiitikio:
Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.
Mashairi. (Zaburi ya 137: 1-3, 6, 8b)
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, mbele ya miungu nitakuimbia zaburi. Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu.
Nitalishukuru jina lako, kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako; kwa maana umeikuza ahadi yako kuliko jina lako lote. Siku ile niliyokuita uliniitikia, ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Ingawa bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali. Ee Bwana fadhili zako ni za milele; usiziache kazi za mikono yako.