1.
    Â
 Barua nimekuandikia mpenzi tulia uisome
 Miaka sasa inasogea sina budi
kukuarifia
 Inatupasa kuliwazia jambo hili la
kufunga ndoa
 Twende kanisani tukapate Baraka
zake Mungu mwenyezi
Â
Chorus   : Nimeamua ni wewe pekee mpenzi wangu sina
mwingine
                  Nimekubali kukupokea mpenzi
wangu nivishe pete
                  Mpenzi njoo tuandamane
                  Pingu za maisha tuzifunge
                  Pokea pete hii ni ishara
                 Ya upendo wangu kwako wewe
                 (Kwa jina la Baba na la mwana Roho
mtakatifu Amina) x2
Â
Â
2.
    Â
Nikitazama jinsi wenzangu
wanavyojongea altareni
Moyo wangu unahuzunika ninapowazia jambo hili
Inatupasa kuishiriki sakramenti hii ya upendo
Tusiwe tu wa kushangilia kwenye harusi za wenzi wetu
Â
3.
    Â
Ni wengi wamenitamania niweze fungua
roho kwao
Najua kwako ni vilevile wengi wanakumezea mate
Wakati sasa umeshafika mpenzi njoo tuweke wazi
Ulimwengu wote utambue mimi nawe kweli twapendana