Jihadharini nao (mjihadhari na) manabii wa uongo (watu) wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo,
Walakini (kwa) ndani ni mbwa-mwitu wakali
Jihadharini na manabii manabii wa uongo
1.Mtawatambua kwa matunda yao x2 – Mtawatambua
  kwa matunda kwa matunda yao
2.Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika
  mibaruti? - Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri,
  Na mti mwovu (mti mwovu) – huzaa matunda mabaya
3.Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala
  mti mwovu – kuzaa matunda mazuri, hauwezi
  kuzaa matunda, matunda mazuri
4.Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa
  motoni – Ndiposa kwa matunda (kwa matunda) yao
  mtawatambua, kwa matunda yao mtawatambua