HEKALUNI TWENDE
1.
   Â
Ni siku njema tena mungu ametujalia pumzi,
Tunaishi tunayo afya twendeni tumwabudu,
Na waumini wote njoni twende nyumbani mwa bwana,
Tuingie
tumsifu kwa shangwe na furaha.
Ni
asubuhi, njema twende (wote) hekaluni
(tumwombe) mahitaji yetu ya kiroho (tupige)
na makofi (tucheze) na kayamba (tuimbe)
nyimbo
tamutamu za kusisimua x2
Â
2.
   Â
Ndege wa angani walia kwa sauti zao tamu,
Kuashiria kumekucha twendeni tumuabudu,
Mashariki tukitazama jua nalo lachomoza,
Kuonyesha
ni siku mpya twendeni tumuabudu.
3.
   Â
Ametulinda siku wiki miezi sasa miaka,
Tuingie nyumbani mwake twendeni tumuabudu,
Ametuvusha na vikwazo vyake muovu shetani,
Tumefika
siku ya leo twendeni tumuabudu.
4.
   Â
Vipaji mbalimbali Mungu akatujalia sisi,
Â
Yatupasa tumshukuru twendeni tumuabudu,
Njoni wapendwa tumuombe neema nazo baraka,
Atuzidishie
ili tumtumikie milele.